Sisi ni nani

Kuhusu EX‑CASFETA USHIRIKA

Historia, Dira, Dhima na Maadili Yetu katika Utumishi na Mshikamano.

Historia ya EX‑CASFETA USHIRIKA

EX-CASFETA USHIRIKA ni umoja wa wahitimu & wataalamu waliowahi kuwa wanachama wa CASFETA katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Mawazo ya kuanzisha EX-CASFETA USHIRIKA yalianza tangu 2005 kwa baadhi ya wahitimu, lakini haikuweza kufanikiwa kutokana na wahitimu wengi kutawanyika na kwenda maeneo mbalimbali kikazi au kihuduma ndani na nje ya Tanzania.

Lakini Mnamo tarehe 03 June 2015, NURU MWAKANYAMALE akiwa Mbeba maono kwa kushirikiana na Viongozi wengine walikuja na wazo la kutengeneza jukwaa au mfumo utakaowaunganisha na kuwaleta pamoja wahitimu wote ili kuendelea kushirikiana kwenye matukio ya kijamii na kushirikishana Fursa za kiuchumi na kazi pamoja na kubadilishana taarifa mbalimbali. Ndipo likaundwa kundi la WhatsApp kwa lengo kufanikisha matarajio na maono waliyokuwa Nayo, hapo ndipo ukawa mwanzo wa Familia ya EX-CASFETA USHIRIKA.

EX-CASFETA tunaamini kuwa kuhitimu chuo si mwisho wa kushirikiana, bali ni mwanzo wa safari mpya ya kujenga na kudumisha ushirika katika kumtumikia Mungu, kusaidiana katika Masuala mbalimbali ya kijamii kama vile misiba, harusi na ugonjwa vilevile kuwa chachu ya maendeleo ya jamii inayotuzunguka kupitia talanta, vipawa, ujuzi na utaalamu wa wanachama Wetu, pamoja na kuunga mkono huduma ya Outreach Gospel Mission (OGM) iliyo chini ya CASFETA TAYOMI Chuo kikuu cha Ushirika Moshi.

Kwa sasa, EX-CASFETA ni familia inayoendelea kukua na kuongezeka, ikijengwa juu ya misingi ya upendo, umoja na mshikamano. Dhamira yetu ni kuwajenga wanachama wake kuwa watu wenye mchango chanya katika Kanisa na jamii, ili kwa pamoja tuwe sehemu ya kuleta maendeleo, matumaini na mabadiliko yenye tija kwa Taifa letu na Ulimwengu kwa Ujumla.

2015

Mwanzo wa CASFETA MoCU

Kutoka kikundi kidogo cha wanafunzi hadi jumuiya kubwa ya kitaifa ya wahitimu.

Dira Yetu (Vision)

"Kuwa jumuiya imara ya wataalamu inayojenga kizazi chenye umoja, maadili ya Kikristo na mchango chanya katika maendeleo ya kiroho na kijamii."

Dhima Yetu (Mission)

"Kuwaunganisha na kuwawezesha wahitimu waliotoka CASFETA kudumisha umoja na mshikamano, kugusa maisha ya jamii inayotuzunguka kupitia huduma za kijamii, kushirikishana fursa za kiuchumi na kazi, pamoja na kuendeleza maisha ya kumtumikia Mungu kupitia kuhubiri injili kwa ajili ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii na kuujenga Ufalme wa Mungu."

Misingi Yetu (Core Values)

Misingi na nguzo tunazosimama nazo katika kila huduma na shughuli ya EX‑CASFETA.

1. Kumcha Mungu

Kuishi kwa maadili ya Kikristo.

2. Upendo na kuhudumiana

Kufanya kila jambo kwa upendo usio na kikomo kwa Mungu na jamii kwa ujumla.

3. Uadilifu na Haki

Kuishi maisha ya uaminifu na kufuata misingi ya kutenda haki kwa watu wote.

4. Umoja na mshikamano

Kushikamana kwa pamoja kama familia bila kujali tofauti Zetu.

5. Huduma kwa Jamii

Kujitoa na Kujitolea kwa moyo katika kusaidia wengine na kuhubiri upendo kwa matendo.

6. Uaminifu na uwajibikaji

Kuwa waaminifu kwa Mungu na jamii & kuishi maisha ya kuwajibika ili kutimiza kusudi la kuwepo kwetu duniani.

Malengo ya EX‑CASFETA USHIRIKA

Kama jumuiya imara, tumejiwekea malengo ya wazi yanayotusaidia kupima mafanikio yetu na kuona matokeo chanya miongoni mwa wanachama wetu:

  • Kudumisha mtandao imara wa mawasiliano na ushirikiano miongoni mwa wahitimu wote wa CASFETA MoCU.
  • Kuanzisha na kuendesha miradi ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya wanachama na jamii kwa ujumla.
  • Kuweka mfumo thabiti wa kusaidiana katika matukio ya kijamii nyakati za furaha na huzuni (kama vile harusi, misiba, Ugonjwa, n.k.).
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu, kushirikishana Fursa za kiuchumi na fursa za ajira au biashara kwa wanachama wetu.
  • Kuendelea kuwa washauri na kuunga mkono CASFETA MoCU kwenye shughuli mbalimbali wanazozifanya.

Muundo wa Uongozi na Majukumu Yake

Umoja wetu unaendeshwa na viongozi wenye maono, weledi na unyenyekevu katika utumishi:

Mwenyekiti
Kiongozi mkuu anayesimamia na kuongoza shughuli zote za EX-CASFETA na kuhakikisha maamuzi ya wanachama yanatekelezwa. Ni Msemaji mkuu wa kundi.
Katibu
Mtendaji mkuu anayesimamia uratibu wa shughuli, mawasiliano na kumbukumbu na nyaraka za EX-CASFETA.
Mhazini
  • Msimamizi wa mapato na matumizi ya fedha za Kikundi
  • Mkusanyaji na Mtunzaji wa michango ya kikundi.
  • Muandaaji wa taarifa za fedha.
  • Mtunzaji wa kumbukumbu za fedha na mfuko wa kikundi.
Wajumbe
  • Wawakilishi wa wanachama na Viongozi wasaidizi kwenye kusimamia na kutekeleza majukumu mbalimbali ya kila siku ndani ya kundi.
  • Wasimamizi wa nidhamu na umoja wa kundi na wajumbe wa kamati ya utatuzi wa changamoto na migogoro ndani ya kundi.
Usajili Uko Wazi

Tayari Kuungana na Jamii ya EX‑CASFETA USHIRIKA?

Jiunge na familia imara ya wahitimu wa CASFETA MoCU leo hii. Ungana na mamia ya wataalamu na viongozi kote Tanzania ili kushirikiana kiuchumi, kijamii na kiroho!